Bishop Dr. Manasse DM
Mchungaji wetu mkuu wa ENCC–Mji wa Bwana.
Utabarikiwa . Utainuliwa . Utafunguliwa . Utaponywa . Utapata Mpenyo na Kutofautishwa Milele
Mji wa Bwana ilianzilishwa 27 Oktoba 2013
27 Oktoba 2013
Kuwapenda watu wote kwa upendo usio na masharti wala ubaguzi. Tunayaishi maagano ya Mungu wa maagano kwa namna isiyo ya kupapasa. Tunajidhabihu kwa sadaka zetu, imekuwa ni maombi yetu na shauku yetu kuwafikia walio mbali kwa vipindi vya TV, redio, mitandao ya kijamii na vipeperushi.
Isayah 25:6–7, na katika mlima huu Bwana atawafanyia mataifa karamu ya vinono. Bwana ameiinua Madhabahu ya Mji wa Bwana na kuuita kwa jina lake. Amechagua kulikalisha jina lake, akisikia maombi ya watu wake wanaomuita tokea mahali hapa, 2 Nyakati 7:15–16. Ni Madhabahu yenye kumdhihirisha Mungu wa kweli kwa ibada zenye mdhihirisho wa matendo makuu ya ishara na ajabu kwa kumwabudu katika roho na kweli, kwa kusifu, kuabudu Neno lililo hai, maombi, kuomba na maombezi. Madhabahu ina mlinzi wa Madhabahu ambaye ni Malaika wa Mungu anayebeba maombi yako na kuyafikisha mbele za Mungu, nawe kuyapokea majibu yako. Zaburi 48:8, kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Mji wa Bwana utaona kama ulivyosikia, shuhuda zake kuu. Utaitwa MJI WA BWANA, Sayuni Mtakatifu wa ISRAELI.